Tetesi za usajili barani Ulaya Ijumaa 2 November 2018
Tetesi za usajili barani Ulaya Ijumaa 2 November 2018
Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 23, ambaye kandarasi yake inamalizika mwisho wa msimu huu, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya hatua ambayo huenda ikatia kikomo shinikizo za mashabiki kutaka kiungo huyo kuondoka klabu hiyo kutokana na utenda kazi wake duni uwanjanani. (Manchester Evening News)
Aaron Ramsey, 27, kiungo wa kati wa Wales, ameambiwa na Arsenal anaweza kuihama klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Mail)
Borussia Dortmund inapania kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City na timu ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 21 Phil Foden, 18. Huenda wakamnunua kwa kima cha euro 175,000. (Mail)
Aliyekuwa meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte bado anapigiwa upatu kuchukua wadhifa wa kuwa mkufunzi mkuu katika klabu ya Real Madrid licha ya tetesi za mapema wiki hii kwamba hakuna uwezekano huo. (AS)
Arsenal na Tottenham wanang’ang’ania kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Malcom, 21, huku mchezaji huyo raia wa Brazil akinyimwa muda wa kucheza katika uwanja wa Nou Camp. (Mundo Deportivo kupitia Mirror)
Kiungo wa Kati wa Denmark Christian Eriksen, 26, anajiandaa kutia saini kandarasi ya kurefusha muda wake Tottenham. (Evening Standard)
Kiungo wa kati wa Chelsea na England Ross Barkley, 24, huenda akawa “Frank Lampard mwingine”, kwa mujibu wa mchezaji maarufu wa zamani wa klabu hiyo Pat Nevin. (Love Sport Radio)
Juventus inatarajiwa kumwinda kiungo wa kati wa Manchester United kutoka Uhispania Juan Mata, 30 mwezi Januari.
Mata anahudumia mkondo wa mwisho wa kandarasi yake katika uga wa Old Trafford. (Evening Standard)
Manchester United ilikasirishwa na lugha chafu iliyotumiwa na kiungo wa kati wa Liverpool na England Jordan Henderson, 28, na wametumia hilo kujitetea kwenye rufaa yao kwa FA kumhusu meneja wake Jose Mourinho (Times)
Wolverhampton Wanderers imehusishwa na tetesi za kumtaka mshambuliaji Liverpool Divock Origi, 23, baada ya kuweka dau lake kwa mchezaji huyo raia wa Ubelgiji wakati wa msimu wa joto. (Birmingham Mail)
Mshambuliaji wa Manchester City na Uhispania U21 Brahim Diaz, 18, huenda akaondoka uga wa Etihad kuelekea Real Madrid. (Telegraph)
Rais wa zamani wa Uefa Michel Platini amesema kiungo wa kati wa Real Madrid na taimu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane, 25, yuko katika nafasi nzuri ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or. (Marca)
Mshambulizi wa Manchester United na England Marcus Rashford amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujumuika na watu wanaosherehekea Halloween. Rashford sasa ana miaka 21. (Manchester Evening News)
No comments: