Ajibu aamua kufunguka kinachoendelea kati yake na Zahera



Ajibu aamua kufunguka kinachoendelea kati yake na Zahera
Kitakwimu ni wazi Asilimia kubwa ya ushindi wa Yanga toka msimu wa ligi kuu Tanzania Bara 2018/2019 umekuwa ukitokana na Kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu.
Kutoa Assist na Kufunga imekuwa ni burudani kubwa anayoitoa Ibrahim Ajibu kiasi cha kuwavutia mashabiki wengi wa Yanga.
Lakini kinyume na mashabiki wengi wa Yanga kocha Mwinyi Zahera amekuwa bado akidiss juu ya uwezo wake akimtoa kasoro nyingi kiasi cha kuzuka kuwa kuna tatizo kati yao.
Lakini Mchezaji huyo Ibrahim Ajibu amefunguka kuwa hakuna tatizo lolote kati yake na Kocha na anaamini anachokifanya kocha lengo lake ni kumtaka aongeze juhudi na kujituma zaidi na si kingine.

No comments:

Powered by Blogger.