Ratiba ligi kuu Tanzania bara TPL Leo 23.09.2018

Image result for makambo yanga

Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea leo kwa jumla ya mechi 4 ikiwemo moja ambayo ilikuwa ichezwe jana kati ya Mwadui na Simba
Mechi ya mapema leo itakuwa kati ya Mbeya City ambao watakuwa wenyeji Sokoine dhidi ya Kagera Sugar mechi ikianza saa nane kamili mchana.
Mechi nyingine itakuwa kati ya Alliance Fc watakaokuwa wenyeji wa Azam Fc CCM Kirumba mechi ikianza saa kumi kamili alasiri.
Nao Mwadui Fc watakuwa mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kambarage kucheza dhidi ya Simba Sc, mechi ikianza saa kumi kamili alasiri.
Na mechi ya Mwisho kwa leo itaanza majira ya saa moja jioni katika uwanja wa Taifa kati ya Yanga wakicheza dhidi ya Singida United kutoka Mkoani Singida.

No comments:

Powered by Blogger.