Alichokisema Mbadala wa Kapombe kuhusu kutua Simba
Simba kwasasa wanahaha kupata beki wa Kulia na baada ya Kuumia kwa Shomari Kapombe hitaji lao kwa beki wa Kulia limekuwa kubwa zaidi.
Kabla ya Kuumia kwa Shomari Kapombe kocha mkuu Patrick Aussems alishaweka wazi kuwa moja ya maeneo anayohitaji wachezaji dirisha dogo ni eneo la beki wa kulia ili kuweza kumsaidia Kapombe kutokana na kutoridhika na uwezo wa Nicolas Gyan katika nafasi hiyo.
Lakini mahitaji ya beki mwingine wa haraka yameongezeka baada ya Kapombe kuumia akiwa na timu ya taifa.
ISHU IKO HIVI SASA KWA BEKI MRITHI WA KAPOMBE.
Inaelezwa kuwa beki wa Tanzania Prisons Salum Kimenya amekuwa kwenye mawindo ya kuwindwa na Simba kwa muda sasa.
Salum Kimenya mwenyewe amefunguka kuwa bado hajasaini Simba kama ambavyo baadhi ya Taarifa zinavyosema lakini amefanya mazungumzo na Viongozi wa Simba lakini bado hawajaafikiana kuhusu Maslahi.
Salum Kimenya amefunguka kuwa ili atue Simba basi ni lazima waweke milioni 90 mezani ndipo asaini kuchezea klabu ya Simba.
Beki huyo ni mwajiriwa wa jeshi la Magereza nchini Tanzania na ameweka wazi kama SImba wangefikia makubaliano basi hata leo angeanza mazoezi na Klabu hiyo.
No comments: