Aussems afunguka kila kitu kuelekea dirisha dogo la usajili



Aussems afunguka kila kitu kuelekea dirisha dogo la usajili
TFF jana ilimtangaza Okwi kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba baada ya kuwashinda wapinzani wake Yahya Zayd na Eliud Ambokile waliofika fainali.
Aussems alisema kuwa licha ya timu yake kufanya vizuri kwenye ligi, bado matamanio yake ni kuwa na kikosi imara zaidi kitakachoweza kupambana kwenye mashindano ya kimataifa.
“Kikosi nilichonacho sasa ni imara na kizuri, tunaweza kupambana na timu yoyote, lakini nataka kuongeza wachezaji wengine kuiimarisha zaidi timu,” alisema Aussems.
Aidha, bila kutaja wachezaji gani anaotaka kuwasajili na kwenye nafasi gani, Aussems alisema ana nafasi nne kwa ajili ya wachezaji wa kimataifa na atazitumia.
Simba inajiandaa na mchezo wake wa kwanza wa hatua ya kwanza ya ligi yamabingwa Afrika ambapo wamepangwa kucheza na Mbambane ya Swaziland ya Burundi kati ya Novemba 27 na 28.
Mabingwa hao wa Tanzania tayari wameshatuma majina ya wachezaji hao kwa Shirikisho la soka Afrika (CAF) huku wakiliengua jina la Nicolaus Gyan kutoka Ghana.
Kuondolewa kwa Gyan kunafanya Simba kuwa na nafasi nne ya kuongeza wachezaji wa kimataifa.
Dirisha dogo la usajili la usajili nchini litafunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15.

No comments:

Powered by Blogger.