Tetesi za usajili barani Ulaya 17.9.2018
Mlinzi wa Manchester united anayetoka Ivory Coast Eric Bailly huenda akaiacha Manchester United mwezi januari ,mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anaoneka kuzivutia timu za Arsenal na Tottenham
Manchester City, Tottenham, Barcelona na Juventus timu zote zinaonekana kumtaka mchezaji wa Paris St-Germain na kiungo wa kati Ufaransa Adrien Rabiot mwenye umri wa miaka 23. (Paris United, via Express)
Kiungo wa Manchester City na Ubelgiji Kelvin de Bruyne anatarajiwa kurudi kuichezea timu yake kwa mara ya kwanza baada ya kuwa majeruhi ,mchezo utakaopigwa tarehe 11 mwezi Novemba.Mchezaji huyo mwenye miaka 27 alitolewa kwenye mashindano baada ya kupata jeraha katika mguu wake wa kulia. (Star)
Meneja wa West Ham,Manuel Pellegrini amekanusha tetesi kuwa Lucas Perez mwenye umri wa miaka 33, alikataa kupasha viungo wakati wa mchezo dhidi ya Everton(London Evening Standard)
Mchezaji wa zamani wa England Stuart Pearce anaamini mshambuliaji wa zamani wa England James Milner 32,ni miongoni mwa wachezaji wazuri katika nafasi yake ya kiungo ndani ya EPL (Talksport)
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 25 amekana madai kuwa hafanyi vizuri kutokana na uchovu alioupata kwenye mashindano ya kombe la dunia
Kiungo wa Wales, Aaron Ramsey, 27 alimuomba kocha wa timu ya Arsenal Unai Emery kumpumzisha katika mchezo dhidi ya Newcastle baada ya kuchoka. (Sun)
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa anajisikia vibaya kwa muda mdogo ambao anapewa kiungo wa England mwenye umri wa miaka 18 na Phil Foden 19, katika msimu huu.
Kocha Aitor Karanka amesema Nottingham Forest itabaki kuwa na subira katika jitihada zao za kumsainisha mshambuliaji Karim Ansarifard mwenye umri wa miaka 28 kwa sababu mkataba wake umesitishwa na Olympiakos. (Nottingham Post)
Mchezaji wa zamani wa Celtic na timu ya taifa ya Scotland, Scott Brown mwenye umri wa miaka 33 amebainisha kuwa alikuwa mbioni kujiunga na Newcastle katika dirisha dogo la usajiri la mwaka 2010.(Newcastle Chronicle)
No comments: