Mbaroni akituhumiwa kumnajisi mwanaye.



Mwanaume mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa kijiji cha Buziba kata ya Nyarugusu mkoani Geita anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuingilia kimwili mara kwa mara mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 6 (pichani). Mwanaume huyo fundi wa baskeli ambaye jina lake halikutambulika mara moja alikuwa akiishi na mtoto huyo baada ya kutalikiana na mke wake kwa muda mrefu.

Chanzo cha kubaini mtoto huyo kufanyiwa ukatili huo ni baada ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Marry Juma kutoa msaada wa kumuogesha mtoto huyo na alipijaribu kumsafisha sehemu za siri mtoto huyo alilalamika maumivu makali na alipojaribu kumhoji mtoto hakuwa tayari kueleza.

Akiendelea kueleza Marry alisema baadaye walimbembeleza mtoto kueleza kipi kilichomsababishia maumivu hayo na ndipo akaeleza kuwa baba yake mzazi huwa anamfanyia kitendo hicho mara kwa mara nyakati za usiku.

Akizungumza na Azam TV mtoto huyo amesema usiku baba yake mzazi amekuwa akimuingilia kimwili na kumsababishia maumivu makali na kudai pamoja na kulia kwa maumivu, huwa hapati msaada kutoka kwa majirani huku baba yake akimtishia kuwa asimueleze mtu yeyote.

Mmoja kati ya majirani katika eneo hilo amesema wamewahi kusiki sauti ya mtoto huyo akilia kwa sauti kubwa majira ya usiku lakini asubuhi walipomuhoji baba wa mtoto, alisema kuwa mtaa huo una washirikina wengi ambao wamekuwa wakimsumbua mtoto hali inayomfanya kuweweseka na kupiga kelele.

No comments:

Powered by Blogger.