FUATILIA MATOKEO | Yanga vs Stand United TPL leo 16.9.2018
Matokeo ya Moja kwa Moja kati ya Yanga ya Dar Es Salaam dhidi ya Stand United kutoka mKoani Shinyanga Live Kutoka Uwanja wa Taifa.
Kuanzia saa kumi kamili Tutakupa KILA kitu Live kaa karibu na wimatz.blogspot.com
Timu zinajiandaa kuingia uwanjani kwaajili ya Pambano
Timu ziko tayari uwanjani na Muda wowote kutoka Sasa PAMBANO litaanza
Mechi Imeanza
Yanga 0 – 0 Stand
Goaaaaaaaaaaal Dakika ya 1 Mrisho Ngassa anaipatia pasi Yanga kwa pasi ya Ibrahim Ajibu
Dakika ya 10
Yanga 1 – 0 Stand United
Yanga wanaonekana kuonana na kuwafurahisha washabiki waliofika uwanjani
Dakika ya 13 Yanga 1 – 0 Stand United
Goaaaaaaal Stand United wanachomoa bao baada ya Movie Nzuri, Goli safi la Alex Kitenge
Yanga 1 – 1 Stand United
Dakika 20
Mechi bado 1 kwa 1 Timu zote zikionekana kushambuliana kwa zamu, Hakuna Mnyonge mpaka sasa
Dakika ya 27 Yanga wanapata Kona , Inachezwa Movie Makambo anapiga Kichwa lakini mpira Unapaa juu ya Lango
Dakika ya 29 Heritier Makambo anamchukua beki anapiga Mpira beki anauzuia ndani ya 18
Dakika ya 30
Yanga 1 – 1 Stand United
Goaaaaaal Ibrahim Ajibu anaipatia Yanga bao la Pili kwa Shuti kaliii nje ya 18, DAKIKA ya 32
Yanga 2 – 1 Stand United
Goaaaaaal dakika ya 35 Andrew Vincent Dante Chikupe anaipatia Yanga bao kwa Goli la Kisigino.
Yanga 3 – 1 Stand United
Dakika ya 37 Mrisho Ngassa anachezewa faulo na anaonekana kuumia , Madaktari wanaitwa Kumtibu
Dakika ya 41 Kichwa alichokipiga Papy Tshishimbi kinagonga mwamba na kurejea uwanjani mabeki wakaokoa.
Yanga 3 – 1 Stand United ( Ngassa, Ajibu, Dante – Alex Kitenge)
Dakika ya 45 Paul Godfrey wa Yanga anapew kadi ya Njano
HALF TIME
Yanga 3 – 1 Stand United ( Ngassa, Ajibu, Dante – Alex Kitenge)
KIPINDI CHA PILI
Kipindi cha Pili kimeanza
Dakika ya 46 Papy Tshishimbi anajaribu shuti kali kwa mguu wa Kushoto mpira Unaenda pembeni ya lango
Dakika ya 55
Yanga 3 – 1 sTAND uNITED
Goaaaaaaaaal Deus Kaseke dakika ya 57 Anaipatia Yanga bao la 4, Assist ya Ibrahim Ajib, Ajib anashiriki kwenye magoli yote manne ya Yanga Leo
Yanga 4 – 1 Stand United.
Goaaaaal dakika ya 59 Stand United wanafunga bao la Pili yuleyule Alex Kitenge
Dakika ya 62 Yanga wanafanya mabadiliko ya KUMTOA Ibrahim Ajibu na Mrisho Ngassa wanaingia Mhilu na Raphael Daud
Dakika ya 63 Makambo anawakosa Stand United kwa mpira wa Kichwa bado ni 4 kwa 2
Dakika ya 71 Feisal Salum anapewa kadi ya Njano
Dakika ya 77 Kelvin Yondani anapewa kadi ya Njano.
Yanga 4 – 2 Stand United
Papy Tshishimbi anapewa kadi ya njano
Dakika ya 79 Refa anaonekana kulaumiwa na washabiki baada ya kuwa na maamuzi yasiyoridhisha
Yanga 4 – 2 Stand United
Kelvin Yondani anashindwa kuendelea na Mchezo na nafasi yake inachukuliwa na Ninja
Dakika ya 85
Bado 4 kwa 2
Full time
Yanga 4 – 3 Stand United
author wima
No comments: