Tetesi za usajili Yanga leo Jumamosi 8 December 2018



Tetesi za usajili Yanga leo Jumamosi 8 December 2018
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema binafsi hana hofu na kiwango cha winga Mkongomani mwenzake, Reuben Bomba lakini atatoa siku mbili sawa na saa 24 kwa kumfanyisha majaribio. 
Bomba anayeelezwa kwamba alikuwa kwenye akademi aliyokuwa mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo ya Ureno alitua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kusajiliwa na Yanga katika usajili huu wa Ligi Kuu Bara unaofungwa Disemba 15, mwaka huu.
Mkongo huyo ameletwa na Yanga kwa mujibu wa mapendekezo ya Zahera aliyoyatoa kwa ajili ya kukiiongezea nguvu kikosi hicho katika mzunguko wa pili wa ligi ingawa bado inaonekana fedha ya kumsainisha ni mtihani.
“Kila mchezaji nitakayemleta ni lazima nimfanyishe majaribio kabla ya kumsajili na kikubwa ninataka kuwaridhisha viongozi uwezo wake kabla ya kumpa mkataba.

“Hivyo, nimetoa siku mbili za kufanya mazoezi ya timu mara baada ya kurejea Dar es Salaam tukitokea Mbeya kucheza na Prisons ambazo ninaamini zinatosha kabisa kuonyesha uwezo wake.

“Binafsi sina hofu kabisa na uwezo wa Bomba ambaye akiwa DR Congo alipata ofa kwenye baadhi za klabu za Ulaya kwenda kucheza soka la kulipwa lakini ilishindikana kutokana na sheria za nchi zilisababisha anyimwe viza,” alisema Zahera. Yanga iko kwenye mazungumzo pia na winga wa Singida, Tibah John na beki Ally Mtoni wa Lipuli.

No comments:

Powered by Blogger.