ofu yatanda baada ya Yondani kutoonekana mazoezini Viongozi wafunguka
Hofu yatanda baada ya Yondani kutoonekana mazoezini Viongozi wafunguka
Klabu ya Yanga imeweka kambi mkoani Morogor ikijiandaa na mchezo dhidi ya Simba utakaofanyika Jijini Dar Es Salaam uwanja wa Taifa 30.9.2018
Lakini jana washabiki waliohudhuria mazoezi ya Yanga waliiingiwa na hofu baada ya nahodha wa Yanga Kelvin Yondani kutoonekana katika mazoezi hayo.
Baada ya mazoezi Moja ya Viongozi wa Yanga kaimu Afisa Habari wa Yanga Godlisten Anderson maarufu kama Chicharito alisema kuwa Yondani alipata matatizo ya Kiafya hali iyomfanya kushindwa kufanya mazoezi hayo na kubakia hotelini.
Hata hivyo kiongozi huyo aliweka wazi kuwa mchezaji huyo anaendelea vizuri na leo huenda akaendelea na mazoezi.
No comments: