Tuesday, April 15 2025

Mtazamo wa Edo Kumwembe timu inayoweza kushinda Simba vs Yanga



Mtazamo wa Edo Kumwembe timu inayoweza kushinda Simba vs Yanga
Leo ndiyo Leo asemaye Kesho Muongo ndiyo msemo unaoweza kuusema kuelekea pambano kati ya Simba na Yanga mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam kuanzia majira ya saa kumi na moja Jioni.
Kuelekea pambano hilo ambalo huvuta hisia za watu wengi kutokana na historia za timu zote mbili zinapokutana.
Moja kati ya wachambuzi wa soka nguli kabisa nchini Tanzania Edo Kumwembe amefunguka kuelekea pambano hilo juu ya timu ambayo inaweza kupata ushindi mbele ya Mwenzake.
Edo Kumwembe akiongea kupitia EFM alifunguka kuwa mechi hiyo haiwezi kuwa nyepesi na kutokana na historia ya timu hizo zinapokutana ni ngumu kuitabiri lakini Matokeo ya Simba siku za karibuni yameiongezea nguvu Yanga kujiamini.
Edo alisema kama mchezo huu ungechezwa wiki 3 zilizopita au nne kabla ya Matokeo ya Ndanda na Mbao kwa Simba basi Ni wazi Simba angekuwa na uhakika zaidi wa kushinda lakini kwasasa Hata Yanga waliokuwa wanachukuliwa poa wanajiamini kutokana na kuanza ligi vizuri na wapinzani wao Simba hawajaanza vizuri sana.
Edo Kumwembe alifunguka pia mechi hiyo itakuwa tamu zaidi eneo la katikati ya uwanja kutokana na aina ya wachezaji waliopo pande zote mbili yani Simba Na Yanga. 

No comments:

Powered by Blogger.