Matokeo TPL Simba vs Yanga Leo 30.9.2018

Matokeo TPL Simba vs Yanga Leo 30.9.2018
Matokeo Ligi kuu soka ya Tanzania bara TPL Leo 30.9.2018 moja kwa Moja kutoka Uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam kuanzia saa 11 Jioni saa za Kenya , Uganda na Tanzania.
TUTAANZA KUKUPA LIVE UPDATES KUANZIA SAA KUMI NA MOJA KAMILI.
Timu zinajiandaa kuingia uwanjani
Mgeni rasmi Job Ndugai yupo uwanjani akisalimiana na wachezaji wa timu zote, akisindikizwa na Waziri Mwakyembe
Filimbi ya Jonesia Rukyaa inapulizwa kuashiria kuanza kwa pambano
Dakika ya 1 Free kick kuelekea Yanga mara baada ya Paul Godfrey kumuangusha Meddie Kagere
Dakika ya 2 Simba wanapata Kona, Inapigwa kona kipa Beno Kakolanya anadaka
Dakika ya 4 Simba wanaonekana kumiliki zaidi mpira zaidi ya Yanga wakipiga pasi za Hapa na Pale kutengeneza nafasi.
Dakika ya 7 Makambo anajaribu kuwachukua mabeki wa Simba na Kisha anapiga Krosi ambayo Gadiel anashindwa kumalizia ilikuwa shambulizi zuri
Dakika ya 11 Beno Kakolanya anaokoa mpira ambao ulipenyezwa na Kichuya kwa Emmanuel Okwi moja ya Shambulizi zuri
Simba 0 – 0 Yanga
Dakika 15 Simba wanapata Kona ya Pili lakini wanashindwa kuitumia bado 0 kwa 0
Dakika ya 16 Okwi anajaribu kupiga shuti mpira Unapaa juu ya Lango
Dakika ya 19 Simba wanawakosa tena Yanga Beno Kakolanya anakuwa Shujaa kwa mara nyingine
Dakika ya 22 Kichuya anapiga shuti linapaa juu ya Lango
Dakika ya 22 Ibrahim Ajibu anajaribu shuti kipa Aishi Manula anadaka mpira.
Dakika ya 23 Kelvin Yondani anapewa kadi ya njano
Dakika ya 26 Simba wanapata Kona Nyingine
Dakika ya 28 Yanga wanapata Kona ya Kwanza ya Mchezo kwa mpira wa Paul Godfrey
Dakika ya 35 Yanga wanafanya shambulizi langoni mwa Simba lakini inakuwa ni Offside.’
Dakika ya 36 Aishi Manula anaonekana kuumia baada ya ya kugusana na mchezaji wa Yanga, anatibiwa na anarejea kama kawa.
Dakika ya 37 Shiza Kichuya anajaribu shuti nje ya 18 Beno anatoa inakuwa Kona
Dakika 40
Simba 0 – 0 Yanga
KIPINDI CHA KWANZA
Kipindi cha kwanza kinamalizika kwa sare ya Bila Kufungana Simba 0 Yanga 0 Simba wakionekana kumiliki zaidi mpira Kuliko Yanga na Kutengeneza nafasi nyingi zaidi ya Yanga.
Simba 0 – 0 Yanga
KIPINDI CHA PILI
Kipindi cha PILI kimeanza
Simba 0 – 0 Yanga
Dakika ya 49 Simba wanafanya shambulizi jingine hatari langoni mwa Yanga, lakini Umakini wa Kagere unakuwa Mdogo inakuwa Goal Kick
Dakika ya 51 Abdallah Shaibu Ninja anaonekana kuwa kisiki kwa washambuliaji wa Simba
Dakika ya 55 Ibrahim Ajibu anatoka anaingia Matheo Anthony
Dakika ya 56 Yanga wanakosa bao la wazi Tshishimbi anawekewa pasi nzuri na Kaseke anapaisha
Dakika ya 58 Matheo Anthony anaonekana kubadili kabisa mpira wa Yanga , Yanga wanaonekana kubadilika na kutengeneza nafasi
Dakika ya 59 Abdallah Shaibu Ninja kidogo ajifunge anatoa inakuwa KONA.
Dakika ya 60 diving header ya Kagere kidogo izae goli kwa Simba Beno anatoa na kuwa Kona
Dakika ya 62 Shiza Kichuya anatoka anaingia Mo Ibrahim
Dakika ya 63 Simba wanafanya shambulizi jingine zito langoni mwa Yanga lakini Beno kwa Mara nyingine anakuwa Shujaa
Dakika 70
Simba 0 – 0 yanga
Dakika ya 71 Pascal Wawa anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea faulo Gadiel Michael
Dakika ya 75 Emmanuel Okwi yupo uwanjani anatibiwa baada ya kuumizana na Paul Godfrey
Dakika ya 77 Shomari Kapombe anajaribu shuti linapaa nje ya 18
Simba 0 – 0 Yanga
Dakika ya 78 Mrisho ngassa anaingia uwanjani kuchukua nafasi ya Deus Kaseke
Dakika ya 81 Cletous Chama aliyeupiga mwingi sana eneo la Kati anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla
Dakika ya 85
Simba 0 – 0 Yanga
Dakika ya 86 Said Ndemla anajigonga akiwa kwenye sita ilikuwa nafasi nzuri kwa Simba kupata Bao.
Dakika 3 za Nyongeza kumalizika kwa pambano la watani wa jadi.
FULL TIME
Simba 0 – 0 Yanga
No comments: