Matokeo Ndanda vs Simba TPL Leo 15.9.2018
Matokeo Ndanda vs Simba TPL Leo 15.9.2018
Haya hapa matokeo kati ya Ndanda Fc kutoka Mtwara dhidi ya Simba ya Kariakoo Dar Es Salaam mechi ya Ligi kuu TPL 2018/2019 MZUNGUKO WA KWANZA.
Dakika kadhaa kutoka sasa Tutakupa Matokeo ya Moja kwa Moja kutoka Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara kati ya Ndanda wana kuchele dhidi ya Simba Mabingwa wa Soka Tanzania bara.
Mechi inachelewa kuanza kutokana na Nyavu kuwekwa sawa
Mechi Imeanza
Ndanda 0 – 0 Simba
Dakika ya nne Simba wanafanya Shambulizi langoni mwa Ndanda lakini SHuti la Mohammed Hussein Zimbwe Jr linakosa kulenga lango.
Dakika 8
Mechi imeanza kwa Kupooza timu zote zinapiga Pasi wanapopata Mpira
Dakika 10
Ndanda 0 – 0 Simba
Dakika ya 18 Mpira Unamiminwa Meddie Kagere anataka kufanya yake lakini anaonekana kukosa Umakinini na Mpira Ule.
Ndanda 0 – 0 Simba
Dakika ya 21 Shiza Kichuya anamimina Krosi upande wa Kushoto lakini kipa wa Ndanda mapema sana anauona mpira ule na Kuudaka
Dakika ya 30 Bado mechi inaonekana kuwa Ngumu kwani mabeki wamekuwa hawaruhusu washambuliaji kupenya kirahisi.
Dakika ya 35 Jonas Mkude anaonekana kuumia yupo nje akitibiwa na Daktari Yassin Jembe.
Dakika ya 39 John Bocco almanusra aipatie Simba bao mpira unaenda nje kidogo tu ya Lango.
Wakati Jonas Mkude akiwa karejea uwanjani Shomari kapombe anaonekana Kuumia na anatolewa nje ya uwanja wakati huo dakika moja ya Nyongeza kukamilisha kipindi cha kwanza
Bado o kwa 0
Kapombe amerejea uwanjani
HALF TIME
Ndanda 0 – 0 Simba
KIPINDI CHA PILI
Tayari kipindi cha Pili kimeanza
Dakika ya 46 Ndanda wanaanza kwa shuti kali la kumtest Aishi Manula lakini Manula anautema na Unarudi uwanjani kabla ya mabeki kuokoa
Ndanda 0 – 0 Simba
Dakika ya 51 Simba wanafanya Shambulizi la maana langoni mwa Ndanda lakini washambuliaji wa Simba wanashindwa kuweka mpira nyavuni.
Dakika ya 56 Shiza Kichuya anapiga free kick inagonga mwamba na Kurudi uwanjani na mabeki wanaosha mpira
Dakika ya 57 Cletous Chama anaingia kuchukua nafasi ya Mo Ibrahim
Ndanda 0 – 0 Simba
Dakika ya 59 Kotei In , Okwi Out
FULL TIME
Ndanda 0 – 0 Simba
FULL TIME
Ndanda 0 – 0 Simba
No comments: