Matokeo Biashara United vs Azam Fc TPL 19.9.2018

Image result for Matokeo Biashara United vs Azam Fc TPL 19.9.2018

Matokeo ya Moja kwa Moja kati ya Biashara United dhidi ya Azam Fc kutoka uwanja wa Karume Musoma Mkoani Mara.
Mechi Imeanza
Biashara United 0 – 0 Azam Fc
Dakika 10 zimekatika katika uwanja wa Karume, Bado 0 kwa 0
Timu zote zinashambuliana kwa zamu huku hakuna timu ambayo imeshatengeneza shambulizi la Kushtua mioyo ya wapinzani.
DAKIKA YA 15
Biashara 0 – 0 Azam Fc
Dakika 25 mechi bado  ni ngumu kwa pande zote , Danny Lyanga yupo chini baada ya kuchezewa faulo na beki wa Biashara.
Biashara 0 – 0 Azam Fc
Dakika ya 30 bado mziki ni mgumu kwa timu zote., 0 KWA 0
Dakika ya 38 Biashara United wanapata kona
Dakika ya 44 Azam wanapiga Kona kuelekea lango la Biashara lakini kipa wa Biashara anaokoa kichwa cha Tafadzwa Kutinyu
Dakika moja ya Nyongeza Kukamilisha kipindi cha Kwanza
Mpira ni mapumziko timu zote zinaenda katika vyumba vya kuvalia matokeo yakiwa bila kwa bila, Kipindi cha Kwanza mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja
HALF TIME
Biashara United 0 – 0 Azam Fc
KIPINDI CHA PILI
Kipindi cha pili kimeanza
Dakika ya 48 Biashara wanafanya shambulizi la hatari langoni mwa Azam FC, lakini wanakosa nafasi hiyo
Biashara 0 – 0 Azam FC
Dakika ya 55 Biashara wanakosa bao la wazi hapa baada ya shambulizi zuri.
Dakika ya 59 Uhuru Suleiman anaingia kuchukua nafasi ya Kaiswa hao ni Biashara United
Wakati huo Yahya Zayd anaingia kuchukua nafasi ya tafadzwa Kutinyu
Biashara 0 – 0 Azam
Dakika ya 68 Anatoka Danny Lyanga anaingia Mbaraka Yusuph, Bado 0 kwa 0
Dakika ya 79 anaingia Kipagwile nafasi ya Singano
FULL TIME
Bishara United 0 – 0 Azam Fc

No comments:

Powered by Blogger.