Zifahamu nguvu za kijeshi Russia na Ukraine

 Mashambulizi ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine yamewashangaza wengi huku wengine wakitamani kujua nguvu za kijeshi za mataifa hayo ya Ulaya Mashariki ambayo yamekuwa kwenye mgogoro kwa miaka kadhaa.

Takwimu zilizotolewa usiku wa jana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky zinaonyesha kwamba watu 137 wameuawa kwenye mashambulizi hayo na wengine 316 wakijeruhiwa.

Nchi hizo zina nguvu kijeshi lakini zinatofautiana kiuwezo kuanzia kwenye bajeti inayotengwa kwenye jeshi, idadi ya wanajeshi, idadi ya wanajeshi wa akiba na aina ya silaha wanazotumia. Hata hivyo, Russia ina nguvu zaidi kuliko Ukraine.

russssianpiic

Jeshi la Russia ni moja ya wanajeshi wenye nguvu zaidi ulimwenguni. Inashika nafasi za juu katika mataifa matano ambayo hutumia fedha nyingi kwenye jeshi lao.

Mwaka 2020, Russia ilitumia Dola 61.7 bilioni kwa ajili ya jeshi lake ambalo lilitumia asilimia 11.4 ya matumizi ya serikali. Kwa upande wa Ukraine, ilitumia dola 5.9 bilioni kwa ajili ya jeshi lake, sawa na asilimia 8.8 ya matumizi ya serikali, kwa mujibu wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI).

Russia ina idadi kubwa ya wanajeshi kuliko Ukraine, hadi sasa ina jumla ya wanajeshi walio kazini 900,000 pamoja na wanajeshi wa akiba milioni 2. Ukraine ina wanajeshi walio kazini 209,000 na wanajeshi wa akiba 900,000.

russian nyinginepic

Kwa upande wa silaha na vifaa vya kijeshi, Russia ina helkopta za mashambulizi 544, mizinga 7571, vifaru 12,420, magari ya kijeshi 30,122 na ndege za kijeshi 1,511.

Ukraine nayo ina helkopta za mashambulizi 34, mizinga 7,571, vifaru 2,596, magari ya kijeshi 12,303 na ndege za kijeshi 98.

Russia tayari imetuma silaha ndani ya umbali wa kushangaza wa Ukraine, ikiwa ni pamoja na mifumo ya makombora ya masafa mafupi ya Iskander, mifumo ya kurusha roketi, vifaru vya kivita na mizinga ya kukokotwa.

russsianpiic

Nchi kadhaa zimetuma vifaa vya kijeshi nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na makombora ya kifaru cha Javelin kutoka Estonia na makombora ya kutungulia ndege ya Stinger kutoka Latvia na Lithuania. Ukraine pia inatumia ndege zisizo na rubani za Bayrakhtar zilizotengenezwa Uturuki.

Ukraine pia imepokea shehena za silaha kutoka Marekani kama sehemu ya kifurushi cha ulinzi cha Dola 200 milioni (£147.5m) kilichoidhinishwa na Rais Joe Biden Desemba mwaka jana.

Ukraine yalipua daraja kuzuia majeshi ya Russia kuingia Kyiv

Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema imelipua daraja la mto wa Teteriv liliopo kaskazini mwa mji wa Kyiv kwa jitihada za kuzuia wanajeshi wa Russia kuvamia eneo hilo. 

Wakati taarifa za kuongezeka kwa idadi ya watu waliofariki baada ya Russia kuivamia Ukraine leo, viongozi mbalimbali duniani wametoa matamko ya kulaani uvamizi huo wakitaka usitishwe mara moja.

Karibu watu 18 na wanajeshi 40 wa Ukraine wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Russia leo Alhamisi Februari 24, 2022 asubuhi katika mji wa Odessa ulio pwani ya Black Sea, serikali imesema. 

No comments:

Powered by Blogger.