Zaidi ya watu 100 wauawa Ukraine
Ukraine imesema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa hadi sasa katika uvamizi wa Russia, huku mapigano yakienea kote nchini na vikosi vya Russia vikisonga mbele kuelekea mji mkuu, Kyiv.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema raia 137 na wanajeshi wameuawa nchini humo katika siku ya kwanza ya uvamizi wa Urusi.
Mashambulizi ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine yamewashangaza wengi huku wengine wakitamani kujua nguvu za kijeshi za mataifa hayo ya Ulaya Mashariki ambayo yamekuwa kwenye mgogoro kwa miaka kadhaa.
Nchi hizo zina nguvu kijeshi lakini zinatofautiana kiuwezo kuanzia kwenye bajeti inayotengwa kwenye jeshi, idadi ya wanajeshi, idadi ya wanajeshi wa akiba na aina ya silaha wanazotumia. Hata hivyo, Russia ina nguvu zaidi kuliko Ukraine.
Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema imelipua daraja la mto wa Teteriv liliopo kaskazini mwa mji wa Kyiv kwa jitihada za kuzuia wanajeshi wa Russia kuvamia eneo hilo.
Katika taarifa yake wizara hiyo imesema wameweza kuzuia majeshi ya Russia kuendelea kuingia kwa kutumia mpaka wa Belarus uliopo umbali wa kilometa 32 kufikia mji mkuu.
Wakati taarifa za kuongezeka kwa idadi ya watu waliofariki baada ya Russia kuivamia Ukraine leo, viongozi mbalimbali duniani wametoa matamko ya kulaani uvamizi huo wakitaka usitishwe mara moja.
Karibu watu 18 na wanajeshi 40 wa Ukraine wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Russia leo Alhamisi Februari 24, 2022 asubuhi katika mji wa Odessa ulio pwani ya Black Sea, serikali imesema.
Taarifa zinasema zaidi ya wanajeshi 40 na raia 10 wamefariki katika saa za mwanzo za uvamizi huo, Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine aliwaambia waandishi
No comments: