Mganga Kataushanga wa Sumbawanga atabiri matokeo mechi Simba na Yanga
Kuelekea pambano la watani wa jadi Simba na Yanga 30 September 2018 Mambo yameanza kuwa mambo mara baada ya joto kuzidi kupanda.
Si unajua mambo ya mila na Desturi za Kiafrika na Tanzania yes ndivyo ilivyo kuna Mganga anayejiita Kataushanga kutoka Sumbawanga ametabiri matokeo ya Simba na Yanga 30.9.2018.
Mganga Kataushanga akiongea kupitia kipindi cha Mshikemshike Viwanjani alisema Simba wananafasi kubwa zaidi ya Kushinda mchezo wa Jumapili kutokana na uwezekano mkubwa wa Mvua kunyesha siku ya Pambano.
Mzee Kataushanga ambaye ni maarufu pia kwa Kutengeneza Mvua lakini pia kwa utabiri wa mambo mbalimbali na taaluma ya Kutengeneza Mvua alisema Ushindi pekee wanaoweza kuupata Yanga ni sare lakini Simba ndiye mwenye nafasi kubwa ya Kushinda kwani Mvua ni dalili njema na ni nyota njema kwa Simba.
Mganga Kataushanga ndiye Mganga aliyeibuka na kusema ndiye aliyesabaisha Mvua wakati Simba inacheza na Al Masry jijini Dar Es Salaam mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 2 kwa 2 akiitaja lengo kama ni kubariki uwanja lakini pia akiamini kuwa Simba ingeshinda mchezo ule kama umeme usingekatika kwani Mvua Tayari ilikuwa ishawabariki Simba.
No comments: