Kikosi : Yanga kitachoivaa Stand United leo 16.9.2018

Image result for makambo

Yanga leo inashuka Dimbani kuwavaa Stand United kutoka Mkoani Shinyanga katika mchezo wa pili kwa YANGA msimu huu wa 2018/2019.
Kuelekea mchezo huo Kocha Mwinyi Zahera ambaye leo atakuwepo kwenye benchi la Yanga kukiongoza Kikosi chake jana katika mazoezi ya Mwisho alionekana kupana Kikosi ambacho kinaonekana kinaweza kuanza leo.
Katika Mazoezi hayo alionekana kumuanzisha Beno Kakolanya Golini.
Beki wa Kulia Paul Godfrey alionekana kupewa nafasi na leo huenda akaanza na hii ni kutokana na Juma Abdul Kurejea mazoezini lakini bado hajawa fiti
Kushoto Zahera alimpanga Gadiel Michael, Huku mabeki wa kati Andrew Vincent na Kelvin Yondani.
Viungo wa Kati 6 na 8, Feisal Salum Fei Toto na Papy Kabamba Tshishimbi walipewa nafasi , Viungo wa pembeni Mrisho Ngassa na Deus Kaseke.
Washambuliji katika mazoezi hayo Heritier Makambo alionekana kuchezeshwa sambamba na Ibrahim Ajiu.
Kikosi kamili Utakipata hapa hapa kitakapotoka Like Ukurasa wetu wa facebook wa rajemuzik

No comments:

Powered by Blogger.