Kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Simba 30.9.2018



Kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Simba 30.9.2018
Kuelekea pambano kati ya Simba na Yanga 30.9.2018 Kocha Mwinyi Zahera katika mazoezi ya Mwisho mkoani Morogoro ameonekana tayari ameanza kutest mipango ya Kikosi chake kitakachoivaa Simba Jumapili.
Katika mazoezi hayo Kipa Beno Kakolanya alionekana kuanza akisaidiwa na Walinzi Paul Godfrey na Gadiel Michael Kulia na Kushoto huku mabeki watatu wenye asili ya Kucheza katikati wakionekana kuandaliwa kucheza kwa pamoja.
Wachezaji hao ni Kelvin Yondani, Andrew Vincent na Abdallah Shaibu maarufu kama Ninja hali inayofanya idara ya Ulinzi kuonekana Kuimarishwa zaidi.
Eneo la Kati Feisal Salum na Papy Tshishimbi walionekana kucheza wakisaidiana na Deus Kaseke huku katika safu ya Ushambuliaji Heritier Makambo akicheza na Ibrahim Ajibu

No comments:

Powered by Blogger.