Huyu ndiye kinda wa Serengeti Boys aliyeitwa Ulaya kwenye majaribio


Huyu ndiye kinda wa Serengeti Boys aliyeitwa Ulaya kwenye majaribio
Wakati Watanzania wengi wakiwa bado wanatambua uwezo wa Timu yao ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17 Serengeti Boys bwana eeh sasa mmoja mmoja wameanza kupata mazali ya kwenda Ulaya.
Nahodha wa timu hiyo Maurice Abraham imethibitishwa na kocha wa timu hiyo Oscar Mirambo kuwa Oktoba 7 atapaa nchini Tanzania kuelekea nchini Denmark kwaajili ya Majaribio
Oscar Mirambo alifunguka kuwa kuna wachezaji wengi wa timu hiyo wameitwa ulaya ila kwasasa viza ya Maurice ndiyo iko tayari.
Maurice Abraham ni moja ya wachezaji waliofanya vizuri katika michuano ya CECAFA iliyofanyika nchini kiasi cha kuwavutia watu wengi.

No comments:

Powered by Blogger.